Kenya Tue 09-12-2008

Kueua Mtoto Msanii
By a Correspondent

Fikiria mchoro wa rangi bila maumbo, mwangaza au kivuli. Mchoro huu hauvutii wala kupendeza. Hakika sio mchoro halisi. Hivyo ndivyo ulimwengu ungalikuwa bila watoto.

Na je chakula ambacho hakina chumvi wala bizari? Hakiliki, hakina ladha. Hii ni taswira ya maisha bila sanaa.

Fikiria ubora wa maisha yenye watoto wasanii... itawezekanaje? Nilizungumza na mwalimu wa shule ya wadudu - watoto wa umri wa miaka miwili hadi miaka sita -  Bi. MaryAnne Marete ambaye ana tajriba ya miaka kumi, na alinidokezea yafuatayo.

Watoto hujifunza kupitia yale wanayoyaona na kuyahisi zaidi ya yale wanayoyasikia. Mandhari ya kwanza ya watoto kujifunza kuhusu maisha, ni nyumbani.

Vile vile somo lao la kwanza la sanaa. Ni jambo la rahisi.  Kama mzazi, unapoanda chakula mezani, kwa mfano matunda,  unaweza kuyapanga kwenye bakuli ama uteo kwa namna ya kuvutia.

Pia, hakikisha mapambo ya nyumba na samani ni ya kuvutia na kusisimua. Isitoshe, vyumba vya kulala vya watoto, vinafaa vikolezwe rangi nyekundu, manjano au samawati na vipambwe kwa vibonzo wanavyopenda.

Ikiwa unaishi katika nyumba ya kukodesha na huwezi kuzipaka kuta rangi nyingine, tumia pazia zenye rangi na michoro ya kuvutia. Sebuleni, picha zilizochorwa na watoto na zilizowekwa fremu zinaweza kuning’inizwa kutani. Hakuna himizo kubwa kwa usanii wa watoto kuliko hili.

Wakati wa mapumziko ndio bora zaidi kwa kukuza usanii. Ni vizuri kuwavumbulia watoto vifaa vya aina nyingi vinavyopatikana nyumbani, kwa mfano makaa, chaki, kalamu zenye rangi na za mate, rangi za maji, matope, ‘mishumaa’, na hata unga wa chapati.

Vyombo vya kupikia pia vyaweza kutumika kama vifaa vya kuchezea, lakini kwa idhini ya mlezi.  Vifaa vyote hivi vinaweza kutumika kuunda maumbo kama ya watu, wanyama, magari, vifaa, nyumba na chochote kile kinachonasa fikira zao. Huu ndio mwelekezo thabiti katika kuchochea usanii.

Bila shaka msomaji waweza kuwa ukijiuliza kwa nini ninatilia mkazo uchocheaji wa usanii katika watoto. Utakubaliana nami kwamba watoto ni tumaini la jamii na hazina la utamaduni. Hivyo basi sanaa itaendelea na kuimarika zaidi ikiwa tutawaridhisha.

Sanaa pia ni njia ya kujieleza kibinafsi. Ni kioo la kuangazia nafsi na tajriba za mtoto, hisia zake, pamoja na miondoko yake ya kimwili.

Bila shaka, ukitaka kujua mitazamo yao ya jamii, chunguza michoro na rangi watoto wanazozitumia. Mathalan, mtoto anayemchora mamaye kama alama ya kituo na mwalimu wake kama kidude kikubwa, anathibitisha umuhimu wa mwalimu wake dhidi ya mzazi wake. Watoto wenye masaibu ya kinyumbani au wenye athari za kiwiliwili wanaweza kujieleza barabara kwa njia ya sanaa.

Tajriba wasizoweza kueleza au kufafanua hufichulika. Hasira na uchungu wa mtoto hubainika ikiwa ametapakaza rangi nyeusi ama nyekundu katika michoro yake. Sanaa inaweza kuwa njia mwafaka ya kutuliza hisia za kutatiza na kuelekeza nguvu na fikra za watoto.

Je, mtoto aliye na kipawa cha kipekee tutamtambuaje? Watoto kama hawa hubainika kwa umbuji walio nao. Katika uchoraji au uundaji hawatumii vifaa walivyozoea au kusomea peke yake, bali wao hutumia chochote kile kinachopatikana.  Mtoto kama huyo,  atachora akitumia vidole, viganja, kucha, nyao, nyuzi, miti, matawi na kadhalika.

Anapoangalia angani, haoni mawingu tu, bali maumbo kama ya ndovu, watu, na vidude vya kila aina. Kueua na kukuza kipawa hiki zaidi, ni muhimu kuwatembeza watoto kuvinjari mandhari, sokoni, maonyesho na mashindano ya kisanaa pamoja na kuwajuliza na watoto wa rika tofauti. Kuwahusisha katika michezo mbali mbali kama kuogelea, kandanda, mbio na nyinginezo huwasaidia katika umbuji.

Ni bora kuwatumbuiza watoto na muziki tofauti kwa sababu hisia zao huathirika kwa njia tofauti na wataibua sanaa za kila aina. Kwa ufupi, siri ya kuvumbua mtoto mwenye kipawa ni kwa kumwelekeza katika hali tofauti za kimaisha. Hata hivyo usimlazimishe mtoto.

Mhimize, msifu na umshauri kwa upole na ustadi. Kwa jumla, mwelekeo wa watoto ni wa matumaini na mafanikio. Ukiwahamasisha vilivyo, utastaajabu matokeo ya sasa na ya vizazi vijavyo.

Wasanii wenye uvumi na walio bingwa sio wa kuzaliwa tu, bali wanaweza kuibuka kwa watoto waliolelewa katika usanii. Msanii Jak Katarikawe – mzaliwa Uganda anayeishi Kenya – ambaye ana maonyesho ya michoro yake katika jumba kuukuu la mkuu wa mkoa wa Nairobi, alijifunza usanii kwa kumuiga mama yake, aliyependa kupamba nyumba yake kwa michoro.

Jitihada unazozifanya wakati huu nyumbani mwako, zinaweza kuchangia kwa kumfanya mwanao msanii mashuhuri katika siku za usoni.

skip to top

Bookmark and Share

Your Comments

Names:

Email:

Commment:

 
skip to top

African Artists Portfolios

Akindiya Olaniyi is a Mixed Media Artist
Dr. Rashid Diab is a Fine Artist
Alemayehu Wariyo is a Fine Artist
Christian Goltz is a Photographer
Enoch Mukiibi is a Fine Artist
Dominique Thoenes is a Fine Artist
Sithabile Mlotshwa is a Mixed Media Artist
Mihret Kebede is a Fine Artist
Tamar Mason is a Mixed Media Artist
Marcela Costa is a Mixed Media Artist
John Kamicha is a Mixed Media Artist
Mia Collis is a Photographer
Willis Otieno is a Mixed Media Artist
Sulaiman  Ishola is a Fine Artist
Xavier Sayago is a Sculptor
Thobias  Minzi is a Fine Artist
Danisile Ncube is a Sculptor
Leon Kuhn is a Mixed Media Artist
Fatric Bewong  is a Fine Artist
Mary Collis is a Fine Artist
Sandi Wells is a Fine Artist
Chokri Ben-Amor is a Fine Artist
Maria Onyegbule is a Fine Artist
Percy Pilane is a Fine Artist
Stephen Garan'anga is a Mixed Media Artist
Veroniccah Muwonge is a Fine Artist
Fitsum Woldelibanos is a Fine Artist
Chiurai Kudzanai is a Mixed Media Artist
Leslie Lumeh is a Fine Artist
Patrick Turkson is a Fine Artist
Click To View All African Artist Portfolios

Kaafiri Kariuki at the Creativity Gallery

Shades of Time: An exhibition by Kaafiri Kariuki at the Creativity Gallery National Museum of Kenya

Editorials By Regions

Featured Artist Portfolio

Title: Making Ways
Name: Tabitha Wa Thuku
Country: Kenya
Medium: Mixed media on heavy canvas
Size: 149 X 140 cms
Click here to view

News

Samuel Githui's 'Zebra Crossing' @ The One Off Gallery
Nomthunzi Mashalaba Presents 'Mamiya'
Portraits for Self Determining Haiti
Word: Future Tense. An Exhibition by Wosene Worke Kosrof
Simon Njami & Ghanaian Architect David Adjaye Collaborate in Visionary Africa: Art at Work

Features

Common Misconceptions Artists Have About Galleries
In Conversation with James Barnor, in Comparison with Malick Sidibé
Gor Soudan & Paul Onditi's 'Another World is Possible'
The Politics of Exclusion: The Undue Fixation of Western-Based African Curators on Contemporary Africa Diaspora Artists-A Critique
An Arts Renaissance in Johannesburg

Editorials

How African Sculpture Influences Modern Art
Interrogating Western Paradigms: Rethinking Authencity in African Art
Should Artists Accept “Dirty Money”?
Art as an Expression: Are artists part of “the problem”?
Development as a Destroyer of Culture: Demolition of Uganda National Museum

News From External Sources

Davidkrut.book.co.za: Special Collection: TAXI Art Book Series
Herald.co.zw: Publishers Challenged to Produce African Art Books
Herald.co.zw: Transforming Colonial Legacy Through Art
Culturemap.com: Faces of Kings
Culture24.org.uk: Brighton Photo Biennial 2010

Exhibitions

Conrad Botes at the KZNSA Gallery

Follow Us On....

Facebook
skip to top

Advertisement

Photo

Newsletter

Advertisement

Partners

Gallery

Connect4climate

 

Advertisement

skip to top
Look

Edcross Fine Art
Art South Africa
Mocada
National Museum Of African Art
Creative African Network
African Art Online
 
Learn

Culture.info
Hivos
Arterial Network
Doen
Blogs

Art's Own Kind
AACHRONYM
Contemporary Arts in Northern Nigeria
Lifestyle & Design

Contemporist
Dwell
Wallpaper*
Cape Craft Design
Moco Loco

Site Map

Contact Us

User Agreement

Privacy Policy

Links & Resources

RSS

FAQ

Home

About Us

Africa Art News

© 2000 - 2010 AfricanColours.
Hosting by Outdare